Putin azungumzia machafuko Ukraine

Haki miliki ya picha .
Image caption Rais Vladimir Putin

Rais Vladimir Putin wa Urusi ameitaka serikali ya Ukraine kusitisha mapigano mashariki mwa nchi hiyo.

Katika mahojiano na gazeti moja la Misri la Al-Ahram kabla ya ziara yake mjini Cairo Misri.

Putin pia ameelezea majaribio ya Kiev kutumia machafuko ukanda huo kama sehemu ya kujiimarisha kibiashara.

Nchi za Magharibi zinailaumu Urusi kwamba imekuwa ikiwasaidia waasi kwa kuwapatia silaha na makundi ya kijeshi lakini Urusi inapuuza madai hayo.

Maoni haya ya Putin kuhusiana na machafuko ya Ukraine yanakuja wakati ambapo Ufaransa na Urusi wanarejesha jitihada mpya za kusitisha mapigano hayo mashariki mwa Ukraine.