Obama na mpango wake kuwashambulia IS

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Barack Obama

Rais Barack Obama ameliomba baraza la Congress kupitisha mpango wa amiaka mitatu wa mashambulizi dhidi ya kundi la wapiganaji wa Kiislam la Islamic State ambalo linashikilia baadhi ya maeneo nchini Iraq. Mpango huo wa Marekani dhidi ya wapiganaji wa IS unahusisha vikosi vya mashambulizi ya ardhini katika jitihada za kutokomeza kundi hilo la kigaidi. Hata hivyo Rais Obama amesema kuwa si kwamba anaomba idhini ya kufanya mashambulizi hayo kwani kwa mjibu wa mamlaka yake hakuna sheria inayoweza kumzuia na kwamba hana nia ya kuendeleza mapigano nchini Iraq bali inamlazimu kufanya hivyo kutokana na vitendo vya IS. Ni mara ya kwanza kwa Rais wa Marekani kuomba idhini ya baraza la Congress ili kutumia majeshi yake tangu utawala wa Rais George W Bush in 2002 pale alipoivamia Iraq