Ajuza awatukana wapiganaji wa IS Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa islamic state

Zaidi ya watu millioni moja katika mtandao wa facebook wameiona video katika mtandao kuhusu ajuza moja kutoka Syria anayewakashifu wapiganaji wawili wa kiislamu akiwaambia ''rudini kwa mungu'' .

Mwanamke huyo aliwakaripia wanaume wawili ambao walikuwa wakichukua kanda hiyo ya video.

''Musiwachinje wenzenu nao pia hawafai kuwachinja''...ni haram...kati yenu na rais Bashar al Asaad hakuna atakayeshinda''.

Hatahivyo watu hao wawili walimjibu wakisema hawana muda wa kupoteza naye ila tu anawafurahisha.

Na baadaye bibi huyo anaonekana akiwaita 'punda',na watu hao wanaonekana wakicheka.

Kanda hiyo ya Video iliwekwa katika mtandao wa facebook na Bint Jbeil,raia wa kusini mwa Lebanon mwenye mtandao ulio maarufu kwa watu wa madhehebu ya kishia.

Mtandao ulidai kwamba ni mama mzee aliyekuwa akiwakosoa wapiganaji wa IS.