Liberia yatangaza kudhibiti Ebola

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais Ellen Jonson Sirleaf wa Liberia ametangaza kwamba Ebola imedhibitiwa nchini humo

Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ametangaza kwamba ugonjwa wa Ebola umedhibitiwa lakini usaidizi zaidi wa jamii ya kimataifa unahitajika kuhakikisha kuwa ugonjwa huo haurudi nchini humo baada ya kuangamizwa.

Ameiambia BBC kwamba kuimarisha mfumo wa afya ni muhimu.

Bi Johnson Sirleaf amekiri kwamba alifanya makosa wakati wa kuzuka kwa ugonjwa huo kama vile kupiga marufuku mikutano ya hadhara bila ya kuwaelezea raia.

Kumekuwa na ongezeko la ripoti za maambukizi mapya katika kipindi cha wiki mbili zilizopita katika mataifa yote matatu yaliokuwa na ugonjwa wa Ebola ikiwemo,Liberia,Guinea na Sierra Leone.

Zaidi ya watu 9000 wamefariki kutokana na ugonjwa huo tangu Disemba mwaka 2013.