Huwezi kusikiliza tena

Nguo za ndani za mitumba bado Uganda

Nguo kuukuu au mitumba bado ni za bei nafuu hususan kwa walala hoi nchini Uganda na maeneo mengine ya Afrika Mashariki. Mbali na kuwa ni za bei nafuu wengi wamekuwa wakizipenda kwa madai kwamba vitambaa vyake ni vya viwango vya juu kuliko vile vinavyotengezwa nyumbani. Biashara ya mitumba katika jiji kuu la Kampala sasa imeshamiri na huenda ikawa ndio kitovu cha biashara katika eneo kanda ya Afrika Mashariki. Mwandishi wetu wa Kampala Siraj Kalyango ametembelea soko la Owino ambalo linasemekana sio tu ni soko kubwa katika kanda ya Afrika mashariki na kati bali pai soko hilo kwa kiasi kikubwa ndiko kunakopatikana nguo kuukuu au mitumba.