Alan Oliveira: Namtaka Oscar Pistorius

Haki miliki ya picha PA
Image caption Alan Oliviera, mwanariadha mwenye ulemavu kutoka Brazil

Mwanariadha mwenye ulemavu Alan Oliveira raia wa Brazil amesema anataka kumuona Oscar Pistorius akirudi katika mchezo wa riadha baada ya kutoka jela.

Pristorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya kuua mpenzi wake Reeva Steenkamp bila kukusudia japo kunauwezekano wa kuachiwa huru mwaka 2015.

"Nataka arudi tukimbie mara nyingi iwezekananyo, nafikiria utakua ni mchuano mzuri tukikutana tena."

"Ni ngumu kwake kurudi katika mchezo itategemea anajisikia vipi,lakini naamini atarudi kucheza na itakua habari njema.

Pistorius aliweka historia katika michuano ya London mwaka 2012 baada ya kukimbia katika michuano ya Olympic ya watu wasio na ulemavu na wenye ulemavu.