Fedha za kukabiliana na ebola zatoweka

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ebola nchini Sierra leone

Ripoti moja imebaini kwamba karibia dola millioni 14 za kugharamia vita dhidi ya ebola nchini Sierra Leone hazijulikani zilipo.

Mkaguzi mkuu amesema kuwa wizara ya afya na kituo cha kitaifa cha kukabiliana na ugonjwa wa ebola zilienda kinyume na sheria.

Mkaguzi huyo amesema kuwa taasisi hizo mbili zilishindwa kutoa stakhabadhi za kandarasi zilizotolewa kununua ambulansi na kujenga kituo cha matibabu ya ebola .

Ripoti hiyo imesema kulikuwa na malipo ya dharura mara mbili kwa wabunge na maafisa wa polisi na kwamba fedha zilipewa watu fulani badala ya mashirika ambayo wangewakilisha.

Serikali haitoa jibu lolote kuhusu ripoti hiyo.