Rais wa zamani kushtakiwa Chad

Image caption Aliyekuwa rais wa zamani nchini Chad Hissen Habre kufunguliwa mashtaka ya uhalifu wa kivita

Mahakama nchini Senegal imeamua kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuweza kumfungulia mashtaka rais wa zamani wa Chad Hissene Habre kutokana na makosa ya uhalifu wa kivita, mateso na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Majaji kwenye mahakama iliyobuniwa na senegal na muungano wa Afrika wamewahoiji zaidi ya mashahidi 2000 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Bwana Habre anashutumiwa kwa mauaji ya maelfu ya watu yaliyoendeshwa kwa misingi ya kisiasa wakati wa kipindi cha miaka minane ya uongozi wake kilichomalizika mwaka 1990.