Rais wa Burundi awaonya waandamanaji

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Burundi

Rais wa Burundi ameonya kuwa watu wanaofanya maandamano watachukuliwa hatua kuwa wachochezi.

Msemaji wa rais, Willy Nyamitwe, alisema hayo kujibu wito wa mashirika ya raia zaidi ya mia 3, kutaka Rais Pierre Nkurunziza, a-si-gombee u-rais kwa muhula wa tatu.

Bwana Nyamwite alisema, ikiwa Bwana Nkurunziza atateuliwa na chama chake, na ikiwa katiba inaruhusu, basi atagombea uongozi.

Ghasia na mvutano unazidi Burundi, kuelekea kwenye uchaguzi wa rais mwezi Juni.