Aliyewashambulia polisi Denmark auawa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maafisa wa polisi wakikabiliana na mtu aliyewashambulia

Polisi kwenye mji mkuu wa Denmark Copenhagen wanasema wanaamini kuwa mwanamume waliyemuua kwa kumpiga risasi ndiye aliyehusika na mashambulizi ya risasi mjini humo.

Polisi wanasema kuwa walimuua mwanamume huyo alipowafyatulia risasi walipokuwa wakipiga doria eneo linalokaribiana na mahala ambapo ufyatulianaji ulifanyika hapo jana.

Saa kadhaa zilizokuwa zimepita mwanamume mmoja myahudi alikuwa ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi wawili kujeruhiwa katika sinagogi kuu mjini Copenhagen.

Siku ya Jumamosi mwanamume mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi kwenye mkahawa mmoja ambapo mjadala kuhusu uhuru wa kujieleza ulikuwa ukifanyika.

Kati ya wale waliokuwa wakihudhuria ni pamoja na mchoraji raia wa sweden ambaye alikuwa amechora vibonzo vya mtume Mohammad akimfananisha na mbwa.