Wataka nguvu za kijeshi kutumiwa Yemen

Haki miliki ya picha AFP
Image caption mataifa ya Ghuba yataka amri ya nguvu za kijeshi dhidi ya waasi wa Houthi kutolewa na baraza la usalama la umoja wa mataifa

Mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka nchi za ghuba wamelitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kuamrisha matumizi ya nguvu za kijeshi nchini Yemen ili kutaua mzozo wa kisiasa uliopo nchini humo.

Mwezi uliopita waasi wa Houthi waliipindua serikali baada ya miezi kadha ya mzozo na rais Abdrabbuh Mansour Hadi.

Majirani wa Yemen wanasema kuwa hayo ni mapinduzi na wanautaka umoja wa mataifa kuingilia kati.

Saudi Arabia na milki ya nchi za kiarabu zimefunga kwa muda balozi zao na kuwahamisha wafanyikazi wao kutokana na sababu za kiusalama.