Mapigano yasita kwa jumla Ukraine

Mpiganaji anayeipendelea Urusi karibu na Debalseve Haki miliki ya picha bbc

Viongozi wa Ufaransa na Ujerumani wamesema wameridhika na namna makubaliano ya kusitisha mapigano yanavyofuatwa kwa jumla mashariki mwa Ukraine.

Walioshuhudia matukio huko wanasema katika maeneo mengi kuna utulivu, ingawa ni utulivu wa wasiwasi, isipokuwa katika eneo la mji wa Debaltseve ambako wapiganaji wanaoipendelea Urusi wameendelea kuwashambulia wanajeshi wa serikali ambao wamewazingira katika mji huo muhimu kwa usafiri.

Hata katika eneo hilo, mapigano siyo makali kama yalivyokuwa.

Shirika la usalama la Ulaya, OSCE, linasema kuwa wapiganaji wamekataa kuruhusu wachunguzi wa OSCE kuingia katika maeneo yao.

Shirika hilo piya linasema makubaliano ya kusitisha mapigano yanafuatwa.

Hatua ya pili ya kurejesha amani ni kwa pande zote mbili kuondosha silaha nzito kwenye mpaka wa mapigano hapo Jumane.