Amani yadumishwa mashariki mwa Ukraine

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Amani yadumishwa mashariki mwa Ukraine kufuatia usitishwaji wa vita

Usitishwaji mapigano unaonekana kudumishwa kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wanaongwa mkono na Urusi mashariki mwa Ukrain.

Eneo hilo limeripotiwa kutulia tangu makubaliano hayo yalipoanza kutekelezwa usiku wa manane saa za eneo hilo licha ya kila upande kumlaumu mwingine kwa kukiuka makubaliano hayo.

Msemaji wa jeshi la Ukrain amesema kuwa wametekeleza mashambulizi wakitumia silaha ndogo katika maeneo tisa huku waasi wakiwalaumu wanajeshi wa Ukrain kwa kuwafyatulia risasi karibu na mji wa Debaltseve.

Mapema rais wa Ukrain Petro Poroshenko alisema kuwa ameamrisha wanajeshi wake kuheshimu makubaliano hayo lakini ameonya kuwa Ukrain haitakimya ikiwa makubaliano hayo yatakiukwa.