Kweli Duniani kuna mambo

John Wojtowicz amekaa kimahamahaba,na ndio maana aliamua kwenda kuiba benki ili alimpie mpenzi wake afanyiwe upasuaji wa kubadili jinsi yake.

Kushindwa kwa jaribio hilo la wizi kulisababisha filamu ya The Dog Day Afternoon kutengenezwa na makala nyingine kibao zikafuatia,na filamu ya hivi karibuni ,The Dog, si ya kimahaba ,lakini yenye kugusa hisia za watu na haina ufiche na yenye kuelezea hali halisi ya mwenyeji wa jiji la New York .

Katika hali ya kawaida hakuna mtu ambaye anaweza kuthubutu kwenda kuiba ama kupora benki ili kufanikisha upasuaji wa kurekebisha maumbile ya mwandani wake ,na ndio sababu iliyolazimu filamu hiyo kutengenezwa anaeleza Wojtowicz ,kwamba katika filamu hiyo The Dog - inamuelezea mwanamume mmoja aliyeamua kujitumbukiza katika kesi mbaya ya wizi katika benki ,tukio ambalo Marekani haijawahi kushuhudia.

Mnamo tarehe ishirini na mbili mwezi August mwaka 1972, John Wojtowicz na wenziwe wawili , Salvatore Naturale na Bobby Westenberg walielekea katika tawi la benki mjini Brooklyn baada ya kushindwa katika jaribio la wizi pia na kutimuliwa kwenye benki nyingine ya Manhattan, wakiwa wamebeba bunduki aina ya shotguns lakini hawakufanikiwa, walishindwa vibaya.

Westenberg hakufanikiwa kupora kiasi kikubwa cha pesa akaamua kutoka, mfanyakazi mmoja wa benki akagundua nusu ya pesa haimo katika kasha la kuhifadhia pesa,mwingine akapiga kengele ya hatari .

Mara eneo lote likazingirwa,wafanyakazi nane wa benki wakageuka kuwa mateka katika kujaribu kujinusuru Polisi nao wakaanza kujadiliana nao ili wawaachilie wafanyakazi hao nao wajisalimishe.

Nje ya jengo watu wapatao mia mbili walikusanyika kushuhudia tukio hilo lililokuwa kama filamu hivi ,tukio lililo husisha FBI , kitengo cha dharura,walenga shabaha mahiri wakiwa juu ya mapaa ya majengo, na wapiga picha za televisheni nao hawakukosa.

Wojtowicz aliicheza nafasi yake kwa umahiri mkubwa, akiwa na madai kadhaa kwa mateka moja wapo likiwa ni chakula kwa mateka ,na akamlipa mleta pizza kiasi kikubwa cha pesa . Akapata mpango, akawarushia mashuhuda wa seke seke hilo ,kwa hilo yeyote angempenda tu.

Saa mbili za majadiliano yao,Wojtowicz akaongeza kiasi cha madai yake kwamba anataka mkewe aliyeko hospitali ya kata ya King's aletwe eneo la tukio. Jina lake ni Ernest Aron. Ni shoga. Nami ni shoga . Hivyo mimi na mke wangu wote ni mashoga