Mapigano yatakoma Mashariki mwa Ukraine?

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mwanajeshi wa Ukraine

Viongozi wa Ujerumani,Urusi na Ukraine wamezungumza kwa njia ya simu zikiwa ni jitihada za kuhakikisha makubaliano ya kukomesha mapigano yanafanikiwa.Pande zote mbili za mzozo zimeshindwa kutekeleza makubaliano kwa muda uliopangwa kuondoa silaha nzito katika mstari wa mbele wa mapambano saa sita usiku.

Msemaji wa Serikali ya Ujerumani amesema kuondolewa kwa silaha kunapaswa kufanyika leo.Msemaji huyo ameeleza kuwa Viongozi hao wamekubaliana kuchukua hatua thabiti kuruhusu waangalizi wa kimataifa kufuatilia kwa karibu shughuli hiyo katika eneo la mapigano.

Halikadhalika wamejadili kuhusu mapigano yanayoendelea mjini Debaltseve.Angela Markel na Petro Poroshenko wamemtaka Rais Vladmir Putin kutowaunga mkono wapiganaji wanaoiunga mkono Moscow.