Ubaguzi wa mashabiki wa Chelsea watolewa

Image caption Paris Mtero

Kanda ya video inayowaonyesha mashabiki wa kilabu ya Chelsea wakimzuia mtu mweusi kuingia katika treni mjini Paris imetolewa.

Katika kanda hiyo mtu huyo anaonekana kujaribu kuingia katika treni hiyo lakini anasukumwa nje.

Kundi moja la watu baadaye linasikika likiimba: ''we are racist,racist and that’s how we like it'' {sisi ni wabaguzi,wabaguzi na hivyo ndivyo tupendavyo}.

Tukio hilo lilifanyika kabla ya mechi ya kilabu bingwa katika mji wa Paris.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mashabiki wa Chelsea

Kilabu ya Chelsea imesema itawasaidia maafisa wa polisi na mashabiki wowote waliohusika watakabiliwa na marufuku.

Kanda hiyo ya video illitolewa na Guardian,ambalo liliripoti kisa hicho kufanyika katika kituo cha Richelieu-Drout katikati ya mji wa Paris siku ya jumanne jioni.

Sauti nyengine ilisikika ikiimba: ''Chelsea,Chelsea,Chelsea''