Waziri mkuu Ugiriki ataka aungwe mkono

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras

Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amesema ameliomba bunge la nchi hiyo siku ya Ijumaa kupiga kura ya kuunga mkono mipango yake ya kumaliza masharti yaliyowekwa kwa nchi yake katika kunusuru uchumi wa taifa hiyo.

Hiyo ni siku ambayo nchi zinazotumia sarafu ya euro zimeweka kama siku ya mwisho kwa Ugiriki kutia saini mkataba unaoipa muda zaidi wa kulipa madeni yake kwa kutakiwa kuheshimu taratibu za matumizi ya fedha.

Hata hivyo maafisa wa Ugiriki wameripotiwa kutaka kuupa Umoja wa Ulaya kuongeza mkataba wa mkopo wake, kama si mpango mzima wa kunusuru uchumi wa nchi hiyo. Habari zinasema bado haijafahamika kama mvutano huu utakubaliwa na EU, ambayo imeiambia Ugiriki kutakiwa kuheshimu makubaliano ya nyuma.

Hadi hapo makubaliano yatakapofikiwa kufikia mwishoni mwa wiki, Ugiriki haitakuwa na fedha. Benki za Ugiriki zinasemekana kuwa na kiwango kidogo cha amana na zimeomba fedha za dharura. Benki Kuu ya Ulaya itaamua Jumatano iwapo iendelee kutoa msaada wa fedha kwa Ugiriki au la.