Waomba mwana wa Wade afungwe miaka 7

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliyekuwa rais wa Senegal Abdoulaye Wade na mwanawe Karim Wade

Waendesha mashtaka nchini Senegal katika kesi inayohusu ufisadi ya mwana wa kiume wa aliyekuwa rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade wameomba ahukumiwe kifungo cha miaka saba gerezani na faini ya dola milioni 430.

Karim Wade analaumiwa kwa kujipatia zadi ya dola milioni 200 kwa njia isiyo halali.

Bwana Wade anasema kuwa alipata utajiri akiwa mfanyi biashara barani ulaya kabla ya kurejea nyumbani ambapo alihudumu kama waziri kwenye serikali ya babake kwa miaka mitatu.