Raia wa Uingereza auawa Sudan Kusini

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sudan Kusini

Muingereza mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa Juba nchini Sudan Kusini.

Makao makuu ya wizara ya mashauri ya nchi za kigeni yamethibitisha kuwa tukio hilo lilifanyika jana jioni katika mji mkuu Juba.

Chanzo cha mauaji hayo hakijulikani.

Mwathiriwa alikuwa akilifanyia kazi shirika moja la kupigania haki za binaadamu la Marekani-Carter Center.

Msemaji wa serikali Ateny Wek Ateny amesema kuwa mtu aliyejihami na bunduki alimfuata hadi katika eneo la shirika hilo na kumpiga risasi kabla ya mtu huyo kutoroka.