Jeshi la Ukraine kuondoka mji wa vita

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wanajeshi wa Ukraine wakijitayarisha kuondoka mji wa Debeltseve

Rais wa Ukraine Petro Poroschenko amesema kuwa majeshi ya Ukraine yanakaribia kumaliza mipango yake ya kuondoka mji wa Debaltseve kuliko na mapigano.

Picha za runinga zinaonyesha milolongo ya vifaru na magari mengine ya kijeshi pamoja na wanajeshi wakiondoka maeneo hayo.

Bado milio ya risasi na mizinga inasikika licha ya kutiwa saini kwa muafaka wa kukomesha vita na kuondoa silaha nzito nzito toka mji huo kutiwa saini juma lililopita.

Rais Poroshenko anasema kuwa kuondoka kwa majeshi yake kumepangwa barabara na amekanusha taarifa kuwa majeshi ya Ukraine, kamwe hayakuwa yamezingirwa.

Sasa anaelekea mashariki mwa taifa ili kuwalaki wanajeshi wake.