Yanga yaongoza ligi kuu Tanzania

Image caption Wachezaji wa Yanga wakishangilia moja ya mabao waliyofunga katika michezo yao ya Ligi Kuu nchini Tanzania

Timu ya Yanga katika Ligi Kuu ya Vodacom imepanda kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuirarua Prisons ya Mbeya kwa mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa Alhamisi jijini Mbeya.

Kwa ushindi huo Yanga sasa inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 28 na kufuatiwa na Azam yenye pointi 26, baada yaambayo kabla ya mchezo wake na Ruvu Shooting ilikuwa ikiongoza ligi hiyo kwa pointi 25.

hiyo iliendelea jana kwa michezo kadha huku vinara wa ligi hiyo Yanga na Azam zikijitupa katika viwanja tofauti.

Katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Yanga walikuwa wageni wa Prisons katika mchezo uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa magoli 3-0.

Na katika mchezo wa Mabatini mkoani Pwani, mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom, Azam walipepetana na Ruvu Shooting. Katika mchezo huo timu hizo ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya kutofungana.

Kwa matokeo hayo sasa Yanga inaongoza msimamo wa ligi kuu ya Vodacom kwa kujikusanyia pointi 28, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 26. Kabla ya michezo hiyo ya Alhamisi Yanga na Azam zilikuwa na pointi sawa yaani pointi 25.

Prisons imeendelea kuzibeba timu zinazoshiriki ligi kuu kwa kujikusanyia pointi 11 tu baada ya michezo 13.

Michezo mingine ya ligi hiyo itaendelea mwishoni mwa wiki katika viwanja mbalimbali, ikiwemo mechi ya timu ya Simba itakayopambana na Stand United mjini Shinyanga.