Thailand yakataza mimba za biashara

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mama aliyepata mtoto kupitia mimba za biashara am'beba mwanawe aliyezaliwa akiwa na ulemavu

Sheria inayowakataza wapenzi wawili wa kigeni wanaotaka kushika mimba kupitia mtu mwengine kwa njia ya malipo imeanza kutekelezwa nchini Thailand.

Sheria hiyo ilibuniwa baada ya wanawake kadhaa nchini Thailand kubeba mimba ya wateja wao wa kigeni.

Haki miliki ya picha Hope for Gammy
Image caption mtoto aliyezaliwa na ulemavu kupitia njia ya ubebaji mimba wa malipo

Kumeshuhudiwa kashfa kadhaa za ubebaji mimba miongoni mwa wateja wa nje ya nchi, ikiwemo kesi maarufu ya wapenzi wawili wa Australia waliomuacha mwana wao wa kiume na mamake aliyemzaa kwa sababu aliyezaliwa na ulemavu, lakini wakamchukua dadake pacha aliyezaliwa bila ya matatizo yote na kumhamisha hadi Australia.

Sheria hiyo mpya haipigi marufuku malipo yote ya ubebaji mimba kwa niaba ya mteja wa kigeni, lakini inafanya kinyume cha sheria matumizi ya mawakala au kupigia debe matangazo ya wanawake wanaotaka kuwabebea wengine watoto.