Liberia yafungua mipaka yake

Afisa wa uhamiaji wa lIberia akagua paspoti ya raia wa Sierra Leone mpakani huku amevaa glovu Haki miliki ya picha European Photopress Agency

Mipaka ya Liberia imefunguliwa rasmi, miezi 7 baada ya kufungwa kwa sababu ya janga la Ebola.

Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, alisema hatua zitachukuliwa kuhakikisha kuwa virusi vya Ebola havitoingia tena nchini kwa kupitia mpakani.

Amri ya kutotoka nje usiku inaondoshwa Jumapili.

Idadi ya watu wanaoambukizwa Ebola nchini Liberia, ni 10% tu ya ilivyokuwa wakati wa kilele cha ugonjwa huo.