Waasi waanza kuondoka Ukraine

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ukraine

Jenerali mmoja wa kijeshi kutoka Urusi aliyehusika katika kutekelezwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano mashariki mwa Ukrain amesema kuwa waasi wameanza kuondoa zana zao kutoka eneo la mapigano.

Jenerali Alexander Lentsov alisema kuwa viongozi wa waasi wametia sahihi amri ya kuondoka eneo hilo ndani ya majuma mawili.

Kuondolewa kwa silaha nzito ambayo ni sehemu ya makubaliano ya wiki iliyopita ya Minsk kulikuwa kumecheleweshwa wakati mapigano yalikuwa yakiendelea sehemu zingine.

Haijabainika iwapo jeshi la Ukrain limekubaliana na hilo.

Mapema pande hizo mbili zilibadilishana wafungwa.