Wakristo watekwa nyara na IS,Syria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wapiganaji wa Islamic State nchini Syria

Wanamgambo wa Islamic State wamewateka nyara watu kadhaa walio wakazi wa Vijiji waishio Watu wa jamii ya kikristo kaskazini Mashariki mwa Syria.

Watekaji waliwakamata Watu hao baada ya kuwavamia na kuwashambulia.katika mazungumzo baina yao kwa njia ya simu Wanamgambo walisikika wakiripoti kuwa wamewateka watu jamii ya kikristo.

Kwa muda sasa jamii ndogo ya kikristo wamekuwa wakiunga mkono vikosi vya kikurdi kupambana na IS.