Je,vipofu huona giza?

Image caption mlemavu wa macho

Mwandishi wa BBC Damon Rose alipofuka alipokuwa mtoto lakini anasema kuwa sio kwamba anaona giza.

Je, yeye anaona nini haswa?.hudhaniwa kwamba watu waliopofuka huona weusi tititi,lakini kulingana na uzoefu wa mwandishi huyu hilo si kweli.

Anasema kwamba kila anapoulizwa ni nini haswa anachokikosa kwa kuwa kipofu yeye husema ni giza.

Anasema kuwa yeye ni mmoja ya watu ambao hawaoni kabisa.

Alipofuka miaka 31 iliopita baada ya kufanyiwa upasuaji ambao haukufaulu.

Image caption Rangi wanazoona watu waliofofuka

Watu hudhania kwamba mwanagaza unapoondolewa basi mtu husalia katika giza.

''Unapoingia katika matandiko huwezi kuona kitu kabisa.Unapofunga macho kila kitu kinabadilika na kuwa giza''.

''Kwa hivyo upofu ni sawa na giza? Inaingia maanani lakini si kweli''.

''Ijapokuwa uhusiano wangu wa akili na macho umekatika duniani haijawa giza kwangu''.

Kwa hivyo unapopofuka ni nini haswa unachoona? aliulizwa mwandishi huyu. ,''jibu ni mwangaza,mwangaza mwingi sana ,rangi za kung'ara,rangi nyingi zinazobadilika kila mara na mwangaza mbaya ulio na bughudha''.