Jeshi la DRC lawashambulia waasi wa FDLR

Image caption Wanajeshi wa DRC wakijitayarisha kuwashambulia waasi wa kihutu wa FDLR

Jeshi nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo limeendesha oparesheni dhidi ya waasi wa Hutu kutoka Rwanda mashariki mwa nchi hiyo.

Kuanza kwa oparesheni hiyo kunatekeleza ahadi ya serikali ya DRC ya kushambulia takriban waasi 1500 wa FDLR baada ya wao kukataa kujisilimishia .

Oparesheni hiyo katika mkoa wa kivu kusini iliendeshwa bila ya msaada kutoka kwa walinda amani wa umoja wa mataifa.

Umoja wa mataifa ulijitoa kutoka kwa operesheni hiyo kwa kuwa jenerali mmoja mkongo ambaye angeshiriki analaumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu.