UK yapitisha Sheria ya mtoto wa wazazi 3

Image caption Uingereza imeidhinisha sheria ambayo mtoto anaweza kuzaliwa kupitia wazazi watatu

Uingereza imekuwa nchi ya kwanza kuidhinisha sheria itakayorusu uzaaji wa watoto wenye vinasaba, DNA kutoka kwa wanawake wawili na mwanamume mmoja.

Sheria hiyo ilioimarishwa imepita kikwazo chake cha mwisho baada ya kuidhinishwa na bunge la taifa hilo.

Sheria hiyo sasa itadhibiti utoaji wa leseni kwa wanaotaka kutengeza watoto hao kwa lengo la kuvilinda vizazi hivyo kutorithi magonjwa mabaya.

Mtoto wa kwanza huenda akazaliwa kabla ya mwaka 2016.

Wabunge wengi katika bunge la Uingereza waliidhinisha sheria hiyo mapema mwezi huu.

Bunge hilo lilipinga jaribio la baadhi ya wabunge 232 kuupinga mpango huo.

Haki miliki ya picha getty
Image caption Mtoto

Katika mjadala,waziri wa afya Lord Howe alisema kuwa kuna fursa ya kutoa matumaini kwa familia.

Alisema kuwa Uingereza inaongoza ulimwengu na kwamba ukaguzi uliofanywa na wataalam unasema kuwa itakuwa salama.

Lord Howe aliliambia Bunge:Familia zitaona kwamba teknologia ipo kuwasaidia na kwamba wako tayari kuikumbatia.

''Itakuwa makuruhu kwa maoni yangu kuwanyima fursa hii.