Waliojaribu kujiunga na IS washtakiwa

Image caption washukiwa waliotaka kujiunga na IS

Wanaume wawili wamefikishwa mbele ya mahakama Jijini New York kwa mashtaka ya kupanga kwenda Syria ili kujiunga na wanamgambo wa Islamic State.

Mmoja wao alikamatwa alipokuwa akijaribu kupanda ndege katika uwanja wa John F Kennedy kuelekea Uturuki, akituhumiwa kuelekea Syria.

Mwanamume wa tatu alifikishwa mahakamani mjini Florida.

Polisi wanasema washukiwa hao wanaotoka Uzbekistan na Kazakhstan, walinuia kutekeleza mashambulio nchini Marekani iwapo wangeshindwa kufika Syria.