Vikombe vya kahawa vinavyoliwa

Image caption Maduka ya kuuza vyakula kote duniani KFC yamezindua kikombe cha kwanza duniani cha kahawa ambacho kinaliwa.

Maduka ya kuuza vyakula kote duniani KFC yamezindua kikombe cha kwanza duniani cha kahawa ambacho kinaliwa.

KFC imezindua kikombe hicho ambacho kimeundwa kutokana na Chokoleti iliyochanganywa na Biskuti.

Vikombe hivyo pia vimewekwa harufu ya kupendeza ya mnazi.

Vikombe hivyo vinavyoitwa ‘’Scoff-ee-cup’’ vinautamu uliyotengenezwa kutoka biskuti ya kipekee iliyofungwa na karatasi ya sukari safi ya chokleti ,inayoweka kahawa kuwa moto.

Lakini baada ya muda chokleti hiyo inaanza kuyeyuka kwa hivyo inakupasa ule ‘’kikombe ‘’chako kwa haraka.

Ikitengenezwa kwa ushirikiano wa wanasayansi maarafu wa vyakula ’’The Robbin Collective’’,vikombe hivyo vya kahawa ambavyo ni asilimia mia

Image caption Maduka ya kuuza vyakula kote duniani KFC yamezindua kikombe cha kwanza duniani cha kahawa ambacho kinaliwa.

mmoja vinaweza liwa zimetengenezwa na harufu nzuri inayoweza kusisimua .

Aidha upishi na viungo vya Robbin collective ‘’siyo tu kuwa vikombe hivyo bali pia vina ladha nzuri mbali na harufu ya kupendeza’’alisema Jocelyn

Bynoe ambaye ndiye meneja wa mauzo wa kampuni hiyo.

Vikombe hivyo vya kahawa vimebuniwa kuadhimisha kahawa nzuri ya ‘’Seattle’’iliyotengenezwa kutokana na kahawa aina ya Arabica .

'Scoff-ee Cups' haziko katika maduka yao kwani bado zinafanyiwa majaribio ya ubora wa bidhaa.