Savile awadhalilisha 63 hospitali

Image caption Jimmy Savile, mtangazaji wa zamani wa BBC

Uchunguzi zaidi kuhusu mtangazaji maarufu wa zamani katika vipindi vya BBC, Jimmy Savile umebaini kuwa aliwadhalilisha watu 63 kutoka hospitali ya Stoke Mandeville, nchini Uingereza, lakini malalamiko rasmi yaliyotolewa kutokana na vitendo hivyo yalipuuzwa.

Uchunguzi huo umebaini kuwa sifa ya Savile kama "mpenda ngono" ilikuwa inafahamika miongoni mwa baadhi ya wafanyakazi, lakini tuhuma hizo huenda hazikuwafikia viongozi.

Malalamiko rasmi yaliyotolewa mwaka 1977 na baba wa muathirika yalitakiwa kuripotiwa polisi, imesema ripoti hiyo.

Ripoti nyingine imesema "matendo ya habari ya Savile " ingeweza kutokea tena.

Ripoti ya Stoke Mandeville imesema waathirika, walidhalilishwa kutoka mwaka 1968-92, walikuwa na umri wa kuanzia miaka minane hadi 40.