Kofi Annan atua Cuba kutatua migogoro

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kofi Annan

Katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan amewasili nchini Cuba kuhamasisha mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Colombia na nchi zenye makundi ya waasi.

Mazungumzo hayo yanayofanyika mjini Havana ni mwendelezo wa hjjitihada za kusaka Amani katika nchi kwa zaidi ya miaka miwili hadi sasa.

Hata hivyo katika mazungumzo hayo ya Amani lengo ni kumaliza migogoro iliyodumu kwa zaidi ya miongo mitano.

Annan amesema atakutana na pande zote mbili za viongozi na kuwa na mazungumzo nao ya pamoja na kwamba atatumia uzoefu wake wa utatuzi wa migogoro katika nchi alizowahi kuwa msuluhishi.