Mwanablogu auawa kinyama Bangladesh

Haki miliki ya picha AVIJIT ROY FACEBOOK
Image caption Marehemu Avijit Roy,mwanablogu aliyeuawa kinyama mjini Dhaka

Mwanablogu mmoja mwenye asili ya Marekani na ile ya Bangladeshi- maarufu kwa maoni ya kumkana Mungu ameuawa kinyama alipozuru mji wa Dhaka.

Avijit Roy - ambaye alikuwa akiishi Marekani - alikuwa amezuru mji huo mkuu wa Bangladeshi na mkewe kuhudhuria dhifa ya uzinduzi wa kitabu.

Alikuwa amepokea vitisho baada ya kuchapisha makala ya kupigia debe maoni huru, sayansi na maswala ya jamii, ambayo yamekuwa yakikosolewa na kutajwa kuwa ni kinyume cha dini ya Uislamu.

Polisi wanasema wanachunguza kuuwawa kwake lakini kufikia sasa hakuna aliyetiwa mbaroni.