Watu 17 wauawa kwa Bomu nchini Nigeria

Image caption Wanamgambo wa Boko Haram wamekuwa wakidhoofisha hali ya usalama nchini Nigeria

Takriban watu 17 wameuawa kwa Bomu la kujitoa muhanga katika kituo cha mabasi mjini Biu, huku mtu mwingine aliyekuwa na nia ya kujitoa muhanga ameripotiwa kukamatwa na Watu na kupigwa mpaka mauti yakamkuta.

Mjini Jos, Watu 15 waliuawa kwa mabomu matatu yaliyorushwa kutoka kwenye Gari katia eneo la kituo cha mabasi na Chuo kikuu.

Uchaguzi wa Urais mwezi Februari umeahirishwa kwa sababu ya machafuko.

Uchaguzi sasa unatarajiwa kufanyika tarehe 28 mwezi March

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, ambaye alikuwa na ziara kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, mjini Baga, amesisitiza kuwa Jeshi linawakabili wanamgambo wa Boko Haram.

Jeshi lilirudisha mji wa Baga kutoka mikononi mwa Boko Haram Wiki iliyopita .Kundi hilo bado linakabili sehemu kubwa ya Kaskazini Mashariki mwa jimbo la Borno na zaidi ya Watu milioni tatu wamekimbia makazi yao.

Mashambulizi mjini Kano na Potiskum siku ya jumanne yaligharimu maisha ya Watu zaidi ya 50.Hakuna kundi lolote lililokiri kutekeleza mashambulizi hayo.