Rinda la Lupita lapatikana

Haki miliki ya picha
Image caption Mwanafilamu aia wa Knya Lupita Nyong'o akiwa amevaa rinda lililodaiwa kuibwa na baadaye kuridishwa katika chumba chake cha hoteli mjini London

Polisi katika jimbo la Los Angeles nchini Marekani wanasema kuwa wamepata nguo wanayoamini iliibwa kutoka kwa chumba cha hoteli cha mwanafilamu raia wa Kenya Lupita Nyongo baada ya kuvaa nguo hiyo wakati wa sherehe za Oscars.

Maafisa hao wa polisi wanasema walipokea habari hizo kutoka kwa mtandao wa watu maarufu TMZ.

Mtandao huo ulipokea simu kutoka kwa mtu aliyedai kuwa alikuwa ameichukua nguo hiyo kabla ya kuirejesha tena hotelini alipogundua kuwa lulu 6,000 ilizokuwa nazo zilikuwa bandia.

Awali nguo hiyo ilikuwa ikidaiwa kuwa na thamani ya dola 150,000.