Gauni ya Lupita ya Oscars yapatikana

Lupita kwenye Oscras na gauni yenye lulu Haki miliki ya picha AFP

Polisi mjini Los Angeles, Marekani, wameweza kulipata lile gauni lilopambwa na lulu, ambalo liliibiwa kutoka chumba cha hoteli cha mchezaji sinema kutoka Kenya, Lupita Nyong'o, ambalo alivaa katika tamasha la Oscars.

Polisi walitomezwa na mtandao wa kijamii, TMZ.

Mtandao huo ulipata simu kutoka kwa mwanamme mmoja ambaye alidai kuwa aliichukua kanzu hiyo na kisha aliirudisha hoteli, baada ya kutambua kuwa lulu 6,000 zilizopambwa juu ya nguo hiyo zilikuwa za uongo.

Hapo awali iliarifiwa kuwa nguo hiyo ilikuwa na thamani ya dola 150,000.