Misri yataka jeshi la pamoja kuundwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Misri Abdel fatah Al Sisi

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ambaye yuko ziarani nchini Saudi Arabia ambapo amarejelea wito wake wa kutaka kuwepo kwa kikosi cha pamoja cha nchi za kiarabu cha kukabiliana na vikundi vya wapiganaji vinavyoendelea kuchipuza katika eneo la mashariki ya kati.

Kwenye mahojiano na kituo cha runinga cha Al Arabiya amesema kuwa anafikira kuwa Saudi Arabia, Jordan na milki ya nchi za kiarabu zinaweza kushirikiana na Misri.

Al Sisi ameipongeza Saudi Arabia na mataifa ya ghuba kwa msaada wao kwa taifa la Misri.