Serikali na waasi kuafikiana Mali

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mali

Serikali ya Mali na makundi sita ya wanamgambo wanatarajiwa kutia sahihi makubaliano ya amani yenye nia ya kuleta utulivu nchini humo.

Chini ya makubaliano hayo wanamgambo hao watajumuishwa kwenye jeshi la Mali na kutumwa eneo la kaskazi mwa nchi .

Vikosi vya ufaransa na vingine kutoka nchi za Afrika vilingia nchini Mali mwezi Januari mwaka 2013 kuzuia kuenea kwa wanamgambo walio na uhusiano na mtandao wa al Qaeda kwenda maeneo ya kusini .

Wanamgambo hao walitimuliwa kutoka miji iliyo kaskazini mwa nchi lakini hata hivyo wale walio wafugaji wa Tuareg na makundi mengine ya kiislamu bado yanaendelea na harakati zao.

Kusainiwa makubaliano hayo kunafanyika baada ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kutoa vitisho vya vikwazo kwa waasi wa Tuareg na makundi yanayoiunga mkono serikali.