Wasichana walioelekea Syria waonekana

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Wasichana wa Uingereza waliotorokea Syria kujiunga na IS waonekana katika kand ya Video

Kanda ya Video ya CCTV imeonyesha picha za wasichana watatu wa Uingereza waliotoroka makwao kuelekea nchini Syria ili kujiunga na wapiganaji wa IS.

Shamima Begum,Amira Abase wenye umri wa miaka 15 na kadiza Sultana mwenye umri wa miaka 16 walisafiri kutoka London kuelekea Istanbul tarahe 17 mwezi Februari.

Picha hizo zimewaonyesha wakisubiri katika kituo cha basi cha Bayrampasa baadaye siku hiyo.

Wapepelezi wa Scotland Yard wanaamini wanafunzi hao wa shule ya Bethnal Green Academy wameingia nchini Syria.

Haki miliki ya picha MET POLICE
Image caption wasichana walioelekea Syria

Wanadaiwa kupokewa mpakani na wapiganaji wa Islamic State.

BBC inaelewa kwamba wasichana hao walingojea katika vituo wiwili vya mabasi kabla ya kuchukua basi la kuelekea Urfa karibu na mpaka wa Syria tarehe 18 Februari.

Kutoka kituo hicho wanadaiwa kupelekwa karibu na kivuko cha mpaka huo na wapiganaji hao.

Wakati katika kanda hiyo ya video unaonyesha kuwa wasichana hao walikaa katika kituo hicho kwa takriban saa 18.