Mapambano yaendelea mjini Tikrit

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Iraq inapambana na Wanamgambo wa Islamic State

Vikosi vya kijeshi vya Iraq vimesema vimedhibiti maeneo kadhaa ya mji wa Tikrit, wakiwa katika harakati za kuurejesha mikononi mwao mwao mji huo kutoka kwa Wanamgambo wa Islamic State.

Wanajeshi elfu thelathini wamekuwa kwenye shambulio hilo wakiwemo kundi la wanamgambo wa kishia linaloungwa mkono na Iran na wapiganaji wa kisunni wa eneo hilo.

Vyombo vya Habari vya Iraq na Iran vimesema Kamanda wa vikosi vya mapinduzi wa Iran alikuwa akiongoza Operesheni hiyo, amefanya kazi muhimu kuwaleta pamoja wapiganaji wa kishia.

Kumekuwa na hofu kuwa wapiganaji wa kishia huenda wakalipiza kisasi dhidi ya jamii ya kisunni iliyo mjini Tikrit baaa ya mauaji yaliyotekelezwa na Wanamgambo wa Islamic State dhidi ya mamia ya askari wapya wa kundi la shia.

Majaribio ya awali ya kurejesha mji wa Tikrit yaligonga mwamba baada ya kupata upinzani mkali.

Mji wa Tikrit upo eneo la kaskazini mwa Baghdad katika njia inayokwenda mjini Mousul , Mji wa pili wa Iraq, na mji mkubwa kudhibitiwa na Wanamgambo.

Marekani imesema haifanyi mashambulizi ya anga kuwaunga mkono mashambulizi yanayofanywa na Iraq mjini Tikrit