Wazazi wajiponza kukataa chanjo ya Polio

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanamgambo wa Taliban wamekuwa wakipinga Chanjo dhidi ya Polio

Mamia ya Wazazi nchini Pakistani wamekamatwa kwa kukaidi kuwaacha watoto wao kupatiwa Chanjo dhidi ya Polio.

Wazazi takriban 471 wanashikiliwa kaskazini magharibi mwa jimbo la Khyber-Pakhtunkwa.

Serikali ya nchi hiyo imesema wataachiwa huru iwapo wazazi watatoa hakikisho kwa njia ya maandishi kuwa watawaruhusu watoto wao kupata chanjo dhidi ya Polio.

Wanamgambo wa Taliban wamekuwa wakipiga vita kampeni za kuhamamisha chanjo ya Polio wakidai kuwa chanjo hiyo inawafanya watu kukosa uwezo wa kuzaa.

Wanamgambo wamefanya mashambulizi dhidi ya Vituo vinavyotoa chanjo hiyo na kuua Wafanyakazi waliokuwa kwenye kampeni hiyo.