Majeshi ya Iraq mbioni kuikomboa Tikrit

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Tikrit ilikuwa mji wa pili baada ya Mosul uliotekwa na Islamic State

Serikali ya Iraq inasema kuwa wanajeshi wake wameanza kampeini ya kuwafurusha wapiganaji wa Islamic State kutoka mji wa Tikrit .

Mji huo mkuu wa jimbo la kaskazini la Salahuddin ulidhibitiwa na wanamgambo wa Islamic state Juni mwaka uliopita.

Serikai inasema kuwa wanajeshi 30,000 wakiwemo wapiganaji 200 wakujitolea wa kisuni pamoja na wakurdi wanaelekea mji wa Tikrit wakisadiwa na ndege za kivita .

Mwandishi wa BBC mjini Baghadad anasema kuwa ikiwa mji wa Tikrit utatekwa na serikali itawezesha wanamgambo wa Islamic State kusukumwa kwenda maeneo ya mbali ya kaskazini hadi mji wa Mosul ambao ndio mji mkubwa

zaidi ulio mikononi mwa wanamgambo hao.

Mji wa Tikrit uko kilomita 150kmKaskazini mwa mji wa mkuu wa Baghdad.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Tikrit ilikuwa mji wa pili baada ya Mosul uliotekwa na Islamic State

Runinga ya kitaifa ya Al-Iraqiya imetangaza ripoti iliyodai kuwa wapiganaji hao wa IS walikuwa wamebumburushwa kutoka viunga vya mji wa Salahuddin nje ya Tikrit lakini habari hizo hazijathibitishwa.

Waziri mkuu Haider al-Abadi alifanya mazungumzo na koo za waSalahuddin kabla ya kutangazwa kwa operesheni hii kubwa zaidi kuwahi kufanyika.

Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa jaribio kama hili kutokea mwaka uliopita operesheni ya kujaribu kuwang'oa IS ilitumbukia nyo'ngo huku mamia ya wapiganaji waliokuwa wakiunga serikali mkono wakiangamia mikononi mwa wapiganaji wa Islamic State.

Tikrit, ni ngome ya aliyekuwa rais wa Iraq Saddam Hussein.