Polisi wamuua mtu asiye na makao Marekani

Image caption Polisi wakipambana na mtu huyo punde kabla ya kumpiga risasi

Polisi mjini Los Angeles, wamempiga risasi mtu mmoja asiyekuwa na makazi.

Katika vurumai iliyonaswa katika mkanda wa video, mtu huyo anaonekana akimenyana na maofisa kadhaa wa polisi katika maeneo Skid Row.

Ghafla polisi waliokuwa wamemdhibiti wanasikika wakiamrisha mtu huyo adondoshe bunduki na punde milio tano ya risasi inasikika.

Msemaji wa Polisi anasema kuwa jamaa huyo alitangazwa amefariki mara tu alipofikishwa Hospitalini huku hakuna taarifa zaidi zilizotolewa.

Kiini hasa cha kupigwa risasi kwa mtu huyo wa mitaani, hakijajulikana, lakini duru zasema kuwa awali polisi walipokea simu kuhusiana na kutokea kwa kisa cha wizi.

Kamanda wa kikosi cha polisi cha Los Angeles Andrew Smith alisema kuwa bwana huyo alijaribu kumpokonya polisi bunduki.

Mwaka uliopita mauaji ya wetu weusi yalisababisha majuma ya maandamano ambapo mali ya thamani isiyojulikana iliharibiwa.