Venezuela yatoa Masharti kwa Marekani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri wa mambo ya nje wa Venezuela Delcy Rodriguez

Serikali ya Venezuela imeipa Marekani muda wa wiki mbili kupunguza idadi ya wanadiplomasia wake walio nchini Venezuela.

Waziri wa mambo ya nje Delcy Rodriguez ametoa kauli hiyo baada ya kukutana Mwanadiplomasia mkuu wa Marekani mjini Caracas.

Waziri huyo amesema ni juu ya marekani sasa kuamua nani kati ya mamia ya wanadiplomasia walio nchini Venezuela arudishwe nyumbani.

Nia imeelezwa kuwa awali ilihitajika idadi ya wanadiplomasia 17 ambao idadi hiyo ina uwiano sawa na wanadiplomasia wa Venezuela walio Marekani.

Mwanzoni mwa mwezi huu Marekani iliweka vikwazo kupata viza za kusafiri dhidi ya Maafisa wa Venezuela ambao Marekani inawashutumu kuwa wamekiuka haki za binaadam na waliojihusisha na vitendo vya rushwa.