Ubakaji :Makala ya BBC yazuiwa India

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Vitendo vya ubakaji viliibua hasira kali na maandamano nchini India

Mahakama nchini India imezuia kurushwa kwa matangazo ya mahojiano na mtu mmoja aliye miongoni mwa genge la wabakaji mjini Delhi kuhusu ubakaji na mauaji.

Mahakama mjini Delhi pia imeweka zuio mahojiano hayo yasitolewe kwenye machapisho, mahojiano hayo yanaelezwa kuibua hasira za Watu wengi nchini India

zuio hilo limekuja wakati Serikali ikitaka maelezo kutoka kwa maofisa wa Jela, ikihoji ni namna gani Mtengeneza filamu wa Uingereza aliruhusiwa kufanya mahojiano.

Habari za ubakaji mjini Delhi ziliushtua ulimwengu. Watu wanne walihukumiwa kunyongwa kwa kosa la kubaka na mauaji dhidi ya Mwanafunzi wa miaka 23.

Mahojiano ya Mtengenezaji wa Filamu huyo Leslee Udwin ni makala iitwayo ''binti wa India'' ilikuwa kwenye mpango wa kurushwa siku ya kimataifa ya Wanawake BBC pia ilipangwa kuruka kupitia Televisheni ya India,NDTV.

Bi Udwin amesema alipata ruhusa ya kufanya mahojiano kutoka kwa Mkurugenzi mkuu wa wakati huo katika Gereza la Tihar na Wizara ya mambo ya ndani mwaka 2013 na kupata ruhusa wiki mbili baadae.

Wazazi wa waathiriwa wa vitendo vya ubakaji wamemuunga mkono Udwin.

Msemaji wa BBC amesema Makala hayo yametolewa kwa ushirikiano na Wazazi wa waathiriwa ikivumbua vitendo vya ubakaji vilivyoushtua ulimwengu na kusababisha maandamano makubwa nchini India wakitaka mabadiliko ya tabia na mitazamo mibovu juu ya Wanawake.