Jihad John hakuwa hivi kabla

Image caption Inasemekana kuwa ndiye muuaji mwenye kiu isokatika

Mwajiri wa zamani wa kampuni ya Uingereza amemuelezea muuaji mwenye kiu isiyo katika wa kundi la Islamic State muuaji "Jihadi John" kama mfanyakazi bora aliyepata kumwona katika kampuni yake.

Jina halisi la muuaji ama chinja chinja huyo Mohammed Emwazi alikuwa na mahusiano mazuri na wafanyakazi wenziwe hata watu wa kawaida,alikuwa mkimya na nidhamu ya hali ya juu hii ni kwa muujibu wa kampuni yenye kujihusisha na masuala ya teknlojia kutoaka nchini Kuwait, na alimwajiri Mohammed akiwa na miaka 21 tu kama muuza bidhaa zake.

Mwajiri huyo wa zamani wa Jihad Jon ameshtushwa na mtu aliyekuwa akimfahamu tabia na mienendo tofauti ni yule aliyekuwa mfanyakazi wake na sasa anaoneshwa ulimwenguni kwenye videos kama muuaji mkuu wa IS.

Emwazi,leo ana miaka 26, inaaminika ameshawaua mateka wa mataifa ya Magharibi wapatao watano miongoni mwao raia wa Uingereza wakiwemo Alan Henning na David Haines.

Bosi huyo wa zamani wa Mohammed ameeleza namna alivyokutana na muuaji huyo, kuwa aliwapelekea barua na wasifu wake kielimu katika mlango wa kampuni yake ,kwahakika anamsifu kuwa ni mfanyakazi bora na wa kipekee waliyewahi kuwa naye.

Na akaonesha mshangao wake kuwa inakuwaje mtu mpole na nidhamu ya hali ya juu tena mcheshi kama yeye anageukaje na kuwa mtu tunayemshuhudia leo katika vyombo mbalimbali kwa matukio mabaya kiasi hiki? Haileti maana na haiingii akilini kuwa ndiye Emwazi ninaye mfahamu, naweza kuamini kuwa aliangukia katika mikono ya watu wabaya aliporejea kwao.!

Emwazi aliacha kazi katika kampuni yangu ghafla tu mwezi wa Apri mnamo mwaka 2010 aliporejea tu mjini London.Taarifa za hivi karibuni kupitia barua pepe zinadai kuwa Emwazi aliwahi kutaka kujiua mara mbili hivi wakati alipokuwa mwanafunzi ,wakati alipotanabahi kuwa kundi la kigaidi la MI5 walikuwa wanamfuatilia sana .

Emwazi aliwahi kuongea na waandishi habari mnamo mwaka 2010 kwamba anajihisi kuwa ni maiti itembeayo.

Emwazi aliwahi kuwasiliana na kundi la uhamasishaji baada ya kufanyiwa mahojiano na maofisa wa kupambana na makundi ya kigaidi juu ya jaribio lake la kutaka kuelekea Heathrow kuelekea kwao Kuwait mwaka 2010.

Katika barua pepealiyoituma kwenye shirika la CAGE ,akidai kuwa kikosi hicho kinamzuia kuishi maisha yake mapya ughaibuni,alikoacha kazi na alikuwa akikaribia kuingia kwenye ndoa.

Wakati ambapo Emwazi alipokuwa hajabainika kuwa ndiye "Jihadi John",wawakilishi kutoka kampuni ya CAGE wanamuelezea kama mtu mwema kuliko wote,mpole ,kijana mnyenyekevu tuliyepata kumfahamu .

Kuna suala ambalo limejitokeza ambalo kijana mmoja aliyewahi kusoma chuo cha London university pamoja na Emwazi ameeleza kuwa chuo chao kilikuwa sumu kwa mazingira ya uanzishwaji magenge ya vijana wa kiislam waliopitukia.