Waamua wakifa ubongo wao ufanyiwe tafiti

Image caption Mchezaji akiweka saini maamuzi yake

Mcheza mpira wa mikono nchini Marekani Steve Weatherford na msakata kabumbu wa ligi ya taifa ya nchi hiyo Sidney Rice wametangaza uamuzi wa kipekee kuwa watachangia ubongo wao kwa wahitaji wa kiungo hicho muhimu kwenye kitengo cha utafiti wa kitabibu pindi watakapo aga dunia hii .

Nguli hao wawili wa NFL wanataka kuwapa kitengo cha utafiti wa magonjwa ya ubongo,hasa katika magonjwa yanayo dhoofisha ubongo wa mwanaadamu yatokanayo na mshtuko wa ubongo .

Rice amefanya maamuzi hayo kwa hiari yake, na msukumo wa moyo wake kutokana na matukio yaliyomtokea akiwa michezoni na mshtuko alioupata viwanjani inakadiriwa kufikia matukio 15 hadi 20 tangu alipoanza kujishirikisha na mpira wa miguu akiwa na umri wa miaka nane tu.

Isivyo bahati sikuwa na elimu ya kutosha juu ya masula ya mshtuko wa ubongo na matokeo yake.naamini ubongo unaofanyiwa utafiti na matabibu unaweza kuwa msaada mkubwa ama hata kuzuia mshituko wa ubongo michezoni.

Wawili hao wanaamini kujitoa kwao na ahadi waliyotoa kunaweza kuwafanya wengine kuwaunga mkono.

Suala la mshtuko wa ubongo linaiathiri Sidney na hata mimi mwenyewe kwa upande wa marafiki zangu wa karibu hasa Junior Seau, ambaye alijiua. Seau, alijiua kwa kujipiga risasi kifuani mnamo mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 43.

Utafiti uliofanywa juu ya ubongo wa Seau ilibainika kuwa alikuwa anakabiliwa na tatizo la ubongo lijulikanalo kitaalamu kama encephalopathy, ama CTE, ambalo hudhoofisha ambalo hutokea hushambulia ubongo na kusababisha mgonjwa asiyejiujua kama anaumwa kuwa mkali na mchokozi ama nusu kichaa.

Wachezaji wa zamani wa ligi ya NFL walio wengi wanaweza kuwa na kesi za madai na wakashinda kwa afya zao baada ya kustaafu zitakazo wagharimu dola za kimarekani bilioni moja .na wengi wa wa chezaji wa ligi hiyo wanakabiliwa na tatizo hilo anaelza Weatherford.

Si wanariadha wa kimataifa peke yao wanaokabiliwa na ajali za ubongo tu , lah zipo sababu nyingi tu ambazo humkabili mtu awaye yote.

Kwa pamoja Rice na Weatherford wanafikiri wachezaji wa ligi ya NFL wameshafanyiwa utafiti wa kawaida wenye matokeo mazuri kugundua kama wako kwenye hatari ya kupata mshtuko wa ubongo lakini kuna kitu cha ziada kinachopaswa kufanyika .