Mafuriko yawaua watu 38 Tanzania

Image caption Mafuriko nchini Tanzania yamewaua zaidi ya watu 38.

Mafuriko mabaya kazkazini magharibi mwa Tanzania yamewaua takriban watu 38.

Maafisa wa polisi wanasema kuwa mvua kubwa na upepo mkali ziliharibu nyumba na kufunga barabara karibu na mji wa Shinyanga na hivyobasi kuzuia oparesheni za kuwanusuru watu.

Wanasema kuwa mamia ya watu wamewachwa bila makao huku zaidi ya watu 60 wakijeruhiwa.

Waandishi wanasema kuwa mimea imeharibiwa na mifugo kuuawa.