Iran:Marekani yapinga msimamo wa Israel

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Barrack Obama wa Marekani na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Rais Obama amepuuzilia mbali onyo alilotoa waziri mkuu wa Israel kuhusu mpango wa Iran wa Nuclear katika hotuba yake tata kwa bunge la Marekani.

Bwana Obama amesema Benjamin Netanyahu alishindwa kutoa suluhisho mbadala kuhusu suala kuu la jinsi ya kuizuia Teheran kutengeza silaha za Nuclear.

Bwana Netanyahu ambaye alialikwa kuhutubia bunge na viongozi wa chama cha Republican alishutumu mkataba uliowekwa kati ya mataifa ya magharibi na Iran na kudai kuwa ni hatari .

Iran imesema kuwa hotuba hiyo ilikuwa ikiudhi na ni ya kujirudia.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani , John Kerry, anatakiwa kusafiri Saudi Arabia leo Jumatano kuhakikishia mataifa ya ghuba kuwa mkataba huo utaimarisha nafasi ya Iran katika eneo hilo.