Mvutano kuhamia Digitali waisha Kenya

Image caption Vituo vinne vikubwa nchini Kenya viliingia kwenye mvutano na Serikali kuhusu kuhamia mfumo wa Digitali

Mvutano kati ya serikali ya Kenya na vyombo vya habari kuhusu kuhamia mfumo wa digitali kutoka analogia ambao ulisababisha vituo vinne vikubwa vya televisheni nchini humo kutorusha matangazo hivi sasa umeisha.

Vituo hivyo vinne, ambavyo mfumo wake wa analogia ulizimwa, vitaanza kurusha matangazo yake tena hii leo usiku kuanzia saa moja kasoro dakika kumi.

Makubaliano hayo yalifikiwa siku ya Jumanne kati ya serikali na vituo hivyo vinne vikubwa vya televisheni nchini Kenya NTV, QTV, KTN na Citizen TV ambavyo vimekubaliwa kurusha matangazo yao jijini Nairobi chini ya mtandao wa Africa Digital Networks (ADN).

Matangazo yao yatapatikana kwa wamiliki wote wa ving'amuzi visivyolipiwa kwa wakazi wa Nairobi na vitongoji vyake.